Mke wa rais wa China atembelea wilaya ya kitamaduni katika Kituo cha sanaa za uigizaji cha Hong Kong
2022-07-01 21:01:49| cri

Mchana wa leo Juni 30, mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan alitembelea Kituo cha sanaa za uigizaji katika Wilaya ya Utamaduni ya Kowloon Magharibi ya Hong Kong, ili kujionea hali ya msingi na historia ya maendeleo ya wilaya hiyo. Bibi Peng Liyuan alifanya mazungumzo ya kirafiki na vijana wanaojitolea wanaotengeneza sanaa ya jadi za karatasi na bidhaa nyingine za kiutamaduni, na ubunifu kwenye ukumbi wa ghorofa ya pili ya kituo hicho.