Shambulizi katika jumba la maduka huko Copenhagen lasababisha vifo na majeruhi
2022-07-04 09:14:51| CRI

Kamanda wa polisi wa mji wa Copenhagen, Denmark Bw. Soren Thomassen amesema watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi la risasi lililotokea katika jumba moja la maduka katika eneo la Amager kusini mwa mji huo.

Kamanda huyo amesema polisi walipokea taarifa za kutokea kwa shambulizi hilo jioni, na mshukiwa mmoja mwenye umri wa miaka 22 alikamatwa nje ya jengo hilo. Polisi wameanzisha msako dhidi ya washukiwa wengine katika eneo zima la Zealand nchini humo, uwezekano kuwa tukio hilo linahusiana na ugaidi haujaondolewa.

Manispaa ya mji wa Copenhagen imezindua mwitikio wa dharura baada ya tukio hilo.