Kampeni za uchaguzi wa rais wa Kenya zaingia katika hatua za mwisho
2022-07-05 08:44:35| CRI

Kampeni za uchaguzi wa rais wa Kenya kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 9 zimeingia katika hatua za mwisho, wakati wagombea wanne wa nafasi hiyo wakitangaza ilani zao kujaribu kuwashawishi wapiga kura milioni 22.1 walijioandikisha, huku kukiwa na utatanishi mwingi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za vyama vingi nchini Kenya, kampeni za wagombea urais zimelenga hali ya kiuchumi ya wananchi, iliyosababishwa na mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira.

Hadi sasa wagombea wanne wametangaza ilani zao, zikitaja vipaumbele muhimu ikiwa ni kufufua uchumi kupambana na ufisadi, na kuwawezesha vijana na wanawake.