Watu sita wauawa kwa kupigwa risasi katika gwaride la kusherehekea Siku ya Uhuru nchini Marekani
2022-07-05 08:54:52| CRI

Watu sita wamethibitishwa kuuawa katika tukio la ufyatuaji risasi lililotokea kwenye gwaride la kusherehekea Siku ya Uhuru katika Bustani ya Highland, pembezoni mwa mji wa Chicago, Marekani.

Taarifa zilizotolewa na maofisa husika katika mkutano na waandishi wa habari zinasema watu wengine 31 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali, 12 kati yao wamejeruhiwa vibaya. Mshukiwa wa shambulizi hilo ametajwa kuwa mwanaume mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 20.

Taarifa pia inasema bunduki moja imegunduliwa katika eneo la tukio na kazi ya kumsaka mshukiwa inaendelea.