Rais wa China apongeza miaka 60 tangu mafanikio ya mapinduzi ya kujipatia uhuru ya Algeria
2022-07-06 08:48:16| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebbourne, kutokana na miaka 60 tangu Algeria kushinda mapinduzi ya kujipatia uhuru.

Rais Xi amesema miaka 60 iliyopita, Waalgeria walijipatia uhuru na ukombozi baada ya kufanya mapambano magumu, huku China ikitoa uungaji mkono na misaada kwa Algeria, na nchi hizo mbili zilianza kuwa na urafiki mkubwa. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeaminiana zaidi katika mambo ya kisiasa, na kupata mafanikio makubwa katika ushirikiano mbalimbali. Ameongeza kuwa anapenda kushirikiana na Rais Tebbourne kukuza mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo katika sekta mbalimbali, ili kunufaisha nchi hizo na wananchi wao.