Jumuiya ya Afrika Mashariki yatoa mafunzo kwa wataalamu kuhusu ujuzi wa maambukizi ya bakteria
2022-07-06 08:57:45| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa mafunzo ya siku 21 kwa wataalam wa afya yenye lengo la kuwapatia ujuzi wa jumla na utaalamu wa kutambua maambukizi makubwa ya bacteria kwenye sampuli za kimatibabu.

Taarifa iliyotolewa mjini Arusha na Jumuiya hiyo imesema mafunzo hayo yana lengo la kuinua uwezo wa wataalamu kutambua usugu wa vimelea vya bakteria dhidi ya dawa za kupambana na vimelea hivyo.

Mafunzo hayo pia yatahusisha ujuzi wa matumizi ya maabara inayohama, na yatawawezesha washiriki kuchakata na kukagua sampuli za kimatibabu kikamilifu, na kutumia njia mbalimbali za kutambua kwa kutegemea aina ya sampuli na ugonjwa unaodhaniwa.