Mashindano ya “Daraja la Lugha ya Kichina” yafanyika nchini Kenya
2022-07-07 15:20:36| CRI

Kipindi cha Daraja kinachokujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kinakufahamisha mambo mbalimbali kuhusu uhusiano, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, licha ya habari za wiki hii zilizohusisha China pamoja na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti kuhusu Siku ya Saba Saba na mahojiano kuhusu mashindano ya lugha ya Kichina nchini Kenya kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi.