Watu wanoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram washambulia gereza nchini Nigeria na kutorosha mamia ya wafungwa
2022-07-07 08:43:02| CRI

Wafungwa wanne wamefariki na wengine 443 wametoroka wakati wa shambulizi lililofanywa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha katika gereza moja mjini Abuja, Nigeria.

Msemaji wa Walinzi wa Magereza nchini humo Abubakar Umar amesema katika taarifa yake kuwa, walinzi watatu wa magereza walijeruhiwa wakati washambuliaji hao walipovamia gereza lililoko eneo la Kuje, kusini magharibi mwa Abuja, jumanne usiku.

Mapema jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria Shuaibu Belgore aliwaambia wanahabari kuwa, washambuliaji hao ni wapiganaji wa kundi la Boko Haram ambao walivamia gereza hilo kuwatorosha wafuasi wao. Ameongeza kuwa wengi wa wafungwa walirejea gerezani hapo na wengine walikamatwa kutoka katika maficho yao.