Msukosuko wa gharama za maisha umewaingiza watu milioni 71 kwenye umaskini
2022-07-08 08:52:51| CRI

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inasema ongezeko la mfumuko wa bei kwenye nchi zinazoendelea kuanzia mwezi Machi, limewaingiza watu milioni 71 kwenye umaskini.

Ripoti hiyo ambayo imefanya uchambuzi kwenye nchi 159 zinazoendelea, inaonesha kuwa ongezeko la bei kwenye bidhaa muhimu tayari limekuwa na madhara kwenye kaya maskini. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni ya Balkan, nchi za eneo la bahari ya Caspian na nchi za Afrika Kusini mwa Sahara.

Ripoti hiyo imesema msukosuko wa gharama za maisha unafanya watunga sera hasa wa kwenye nchi maskini wawe na machaguo magumu. Wakati nchi hizo zikikabiliwa na kupungua kwa mapato na kuongezeka kwa madeni, changamoto kubwa iliyopo ni namna ya kuwasaidia maskini na kaya zilizo kwenye hatari.