Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza ufuatiliaji mkubwa kuhusu hali nchini Ukraine
2022-07-08 08:53:55| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, jana alipohudhuria mkutano wa kundi la nchi 20 nchini Indonesia, alibadilishana maoni na mwenzake wa India Bw. Subrahmanyam Jaishankar kuhusu mgogoro wa Ukraine.

Bw. Wang alieleza mambo matatu yanayofuatiliwa na China kuhusu mgogoro wa Ukraine, kwanza inapinga kuufanya mgogoro huo kuchochea wazo la vita baridi na kujenga makundi yanayopingana, pili inapinga kutumia vigezo viwili kudhoofisha hali ya kujiamulia mambo na ukamilifu wa ardhi ya China, na tatu China inapinga kitendo chochote cha kuzuia haki halali ya nchi nyingine kujiendeleza.

Amesema baadhi ya nchi zinatumia mgogoro wa Ukraine kuwa kisingizio cha kuweka vikwazo vya upande mmoja dhidi ya China na nchi nyingine, hatua ambazo amezitaja kuwa zinadhoofisha ushirikiano wa kawaida kati ya nchi na nchi, na zinaharibu kanuni za biashara ya kimataifa na kuchochea zaidi mgogoro wa Ukraine.