Rais mpya wa Sri Lanka kuchaguliwa Julai 20
2022-07-12 10:34:20| CRI

Spika wa bunge la Sri Lanka Bw. Mahinda Yapa Abeywardena amesema kuwa viongozi wa vyama vya siasa wameamua kumchagua rais mpya tarehe 20 mwezi Julai kupitia kupiga kura bungeni.

Kwenye taarifa yake Spika Abeywardena amesema baada ya kukutana na viongozi wote wa vyama vya siasa, wameamua kuitisha kikao cha Bunge tarehe 15 mwezi Julai na kuliarifu bunge kuwa kuna nafasi ya wazi ya urais.

Uteuzi wa wagombea wa kiti cha urais utafanyika tarehe 19 mwezi Julai, na kura za kumchagua rais mpya zitapigwa Julai 20.

Viongozi wa vyama pia wameamua kuunda serikali ya mseto itakayojumuisha vyama vyote chini ya rais mpya na kuchukua hatua kuendeleza usambazaji wa huduma muhimu.

Rais Gotabaya Rajapaksa wa Sri Lanka Jumamosi alitangaza kuwa atajiuzulu kesho Jumatano kutokana na kuyumba kwa uchumi na hali ya kisiasa.