Uganda yaadhimisha Siku ya kupambana na ufisadi ya Afrika
2022-07-12 10:36:49| CRI

Uganda Jumatatu iliadhimisha Siku ya kupambana na ufisadi ya Afrika, inayoangukia tarehe 11 mwezi Julai kila mwaka.

Idara ya Ukaguzi ya Serikali ya Uganda inayoshughulikia kupambana na ufisadi ilitoa taarifa ikisema maendeleo yamepatikana katika kupambana na vitendo hivyo, ingawaje juhudi zinahitajika zaidi kufanywa kwenye mapambano hayo.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Mapambano zaidi dhidi ya ufisadi barani Afrika: Kufuatilia fedha za janga la COVID-19”.

Taarifa hiyo pia ilisema idara ya ukaguzi imepokea na kushughulikia kesi zaidi ya 41 zinazohusika na ufisadi wa fedha za COVID-19, ambapo baadhi za kesi zimefunguliwa mashtaka, baadhi ya fedha zimepatikana, baadhi ya watu wamekamatwa, na kesi nyingine zinaendelea kushughulikiwa.