Kenya yatoa chanjo milioni 19 za COVID-19
2022-07-14 11:12:18| CRI

Wizara ya Afya ya Kenya imesema kuwa imetoa jumla ya dozi milioni 19.01 za chanjo ya COVID-19 na miongoni mwa dozi hizo, milioni 16.8 zimetolewa kwa watu wazima na nyingine kwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 18, huku nchi hiyo ikijitahidi kufikia lengo lake la kutoa chanjo kwa watu milioni 27.2.

Kulingana na wizara hiyo, jumla ya dozi 535,000 za nyongeza pia zimetolewa. Hadi sasa watu wazima milioni 8.7 na vijana 369,835 wamepigwa chanjo kamili.

Hadi sasa nchi hiyo imepokea chanjo milioni 27.8 zikiwemo Moderna, Astrazeneca, Sinopharm, Johnson & Johnson, na Pfizer.