Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa uzinduzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mtandao wa Internet uliofanyika Jumanne mjini Beijing.
Kwenye salamu zake, Rais Xi amesema kufanyika kwa Mkutano huo ni hatua muhimu inayolingana na mkondo wa maendeleo ya zama, na kukuza mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya mtandao. Amesisitiza kuwa mtandao unahusisha hatma ya binadamu, na mustakabali wa mtandao unapaswa kuanzishwa na nchi mbalimbali duniani kwa pamoja. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa, kuhimiza ujenzi wa mtandao wenye haki, utulivu, usalama na uhai ambao unafungua mlango, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi zote duniani.