AU yatuma polisi wapya 160 ili kuimarisha usalama nchini Somalia
2022-07-15 09:34:17| CRI

Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema kuwa imetuma polisi 160 kutoka Nigeria kusaidia juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia.

Mkuu wa kikosi cha kumi na moja cha Polisi Kilichoundwa Na Nigeria (NFPU) Bw. Mohammed Ibrahim amesema kuwa polisi hao ambao wamefunzwa vyema na wana nidhamu, watalisaidia Jeshi la Polisi la Somalia kulingana na Mpango wa Mpito wa Somalia.

Ameongeza kuwa polisi hao pia wataongeza nguvu katika uwezo wa kutoa huduma wa polisi wa Somalia kote nchini na kuwasaidia kupambana na itikadi kali na machafuko ya kijamii kupitia polisi jamii, usimamizi wa utaratibu wa umma, na mikakati mingine ya kuzuia uhalifu.