Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi mjini Urumqi mkoani Xinjiang
2022-07-15 09:29:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi katika chuo kikuu cha Xinjiang, bandari kavu ya kimataifa ya Urumqi, eneo la makazi ya Guyuanxiang lililopo wilaya ya Tianshan na jumba la makumbusho la mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang, kuanzia Jumanne mchana hadi Jumatano asubuhi.

Katika ukaguzi wake rais Xi amefahamishwa mambo mbalimbali yakiwemo kazi ya kukuza vipaji, kuratibu mapambano ya UVIKO-19 na maendeleo ya uchumi na jamii, kuhimiza umoja na maendeleo ya makabila madogo, na kuunganisha hisia za jamii kwa ajili ya taifa la China.

Rais Xi amesema kazi nyingi zinahitaijika kufanywa kwa kutegemea jamii mbalimbali na kuzitaka mamlaka kuongeza juhudi kwenye kazi za ngazi ya jamii ili kujua matatizo yao na kutimiza mahitaji ya watu. Sambamba na hilo, ametoa wito wa kuimarisha mashirika ya chama katika ngazi ya jamii na kuboresha huduma zake ili kuwanufaisha wakazi wa makabila yote madogo.

Wakati huohuo rais Xi amesema wakati ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ukiboreka zaidi, sasa Xinjiang sio tena pembe ya mbali na bali imekuwa eneo muhimu na kitovu cha msingi. Amebainisha kuwa maendeleo makubwa yamepatikana tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” litolewe, hivyo amewaambia wafanyakazi wa bandari kavu kwamba kazi yao ina umuhimu mkubwa na kuwahamasisha kufanya kazi kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi.