Rais Xi Jinping asisitiza kuujenga Mkoa wa Xinjiang uwe na masikilizano, ustawi, na mazingira mazuri ya kiikolojia
2022-07-17 19:31:13| cri

Julai 12 hadi 15, rais Xi Jinping wa China alifanya ukaguzi mkoani Xinjiang na kuwatembelea wananchi wa makabila mbalimbali.

Wakati wa ukaguzi huo, rais Xi amesisitiza kuwa, ni muhimu kutekeleza kithabiti maagizo ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, kutekeleza kikamilifu mkakati wa Chama hicho wa uendeshaji wa mkoa wa Xinjiang katika zama mpya, kushikilia imara lengo kuu la utulivu wa jamii na usalama wa kudumu, kufuata msingi wa kazi wa kutafuta maendeleo chini ya hali ya utulivu, kukuza kwa pande zote mageuzi na ufunguaji mlango, kuhimiza maendeleo ya hali ya juu, kuratibu kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuratibu maendeleo na usalama, ili kujenga Mkoa Mzuri wa Xinjiang wenye masikilizano, ustawi, maendeleo, na mazingira mazuri ya kiikolojia ambao watu wanaishi na kufanya kazi kwa amani .