Sudan yafungua tena kivuko cha mpaka na Ethiopia
2022-07-18 08:25:44| CRI

Sudan imefungua kivuko cha Galabat kwenye mpaka wa nchi hiyo na Ethiopia ili kujenga imani na kutatua mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan limetoa taarifa ikisema, hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za viongozi wa nchi hizo mbili kushughulikia masuala ya mpaka.

Baraza hilo pia limeamua kuongeza ufuatiliaji mpakani na kuboresha uratibu kati ya nchi hizo mbili ili kuzuia watu wenye silaha kuvuka mpaka.

Tarehe 26 Juni, Sudan ilifunga kivuko cha Galabat, ikisema kuwa jeshi la Ethiopia liliwaua wanajeshi saba na raia mmoja wa Sudan kwenye mpaka wa pamoja wa mashariki, madai ambayo Ethiopia iliyakanusha.

Tangu mwezi Septemba mwaka 2020, mpaka wa Sudan na Ethiopia umekuwa ukishuhudia kuongezeka kwa mvutano na mapigano mabaya kati ya nchi hizo mbili.