Mapato ya biashara ya nje ya Ethiopia katika mwaka wa fedha uliopita yafikia dola za kimarekani bilioni 4.12
2022-07-18 08:28:16| cri


 

Wizara ya Biashara na Ushirikiano wa Kikanda ya Ethiopia (MoTRI) hivi karibuni imesema, kipato cha nchi hiyo kutokana na mauzo ya nje ya bidhaa za nchi hiyo kimefikia dola za kimarekani bilioni 4.12 katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 uliomalizika tarehe 7 mwezi Julai.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, mapato ya uuzaji wa bidhaa kwa nje katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 yalifikia bilioni 3.62, huku mapato hayo katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 yaliongezeka kwa dola za kimarekani milioni 500.

Taarifa hiyo pia ilisema sekta ya kilimo ilichangia asilimia 72 katika mapato hayo.