Mwenyekiti wa ECOSOC asema uzoefu wa China katika kuondokana na umaskini unastahili kuigwa
2022-07-18 08:25:49| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) Collen Vixen Kelapile hivi karibuni amesema, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu maskini duniani kufuatia janga la COVID-19, mabadiliko ya tabianchi na mapambano ya kikanda, nchi husika zinapaswa kujifunza uzoefu wa China katika kuondokana na umaskini.

Bw. Kelapile amesema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa wa Mwaka 2022 uliofungwa Ijumaa iliyopita huko New York. Amesisitiza kuwa, kutokomeza umaskini ni lengo la watu wote, pia ni lengo kuu la Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030. Ameongeza kuwa, kufahamu mafanikio ya nchi mbalimbali katika kupunguza umaskini, kunaweza kutia moyo nchi husika kujitahidi kwa ajili ya kutimiza lengo hilo.