Mkutano wa AU wamalizika kwa kutoa wito wa kuongeza maingiliano na kuchochea mageuzi ya kiviwanda
2022-07-18 08:24:28| CRI

Mkutano wa nne wa katikati ya mwaka wa uratibu wa Umoja wa Afrika (AU) umemalizika jana Jumapili mjini Lusaka, Zambia, kwa kutoa wito kwa nchi wanachama kuongeza kasi ya mchakato wa maingiliano na kuboresha ubora wa bidhaa ghafi kupitia mageuzi ya kiviwanda.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Senegal, Macky Sall amewaambia wanahabari kuwa, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja huo wamekubali kutekeleza kihalisi makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) ili kuboresha biashara na kuimarisha maingiliano.

Amesema kwa muda mrefu, Afrika imekuwa ikiuza nje malighafi, na kuongeza kuwa wakati umefika kwa kubadilisha mfumo kwa kuhakikisha kuwa bara hilo linaanza kuongeza thamani ya malighafi zake.