Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kuchukua hatua yenye uratibu kwa mzozo wa chakula duniani
2022-07-19 08:49:11| cri


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alitoa wito wa kuchukua hatua za ujasiri na uratibu ili kupunguza mzozo wa chakula unaoendelea duniani.

Bw. Guterres alisema, hii ina maana ya kurejesha haraka uzalishaji wa chakula wa Ukraine, na chakula na mbolea kutoka Russia, katika masoko ya dunia, na kuendeleza biashara ya kimataifa.

Pia amesisitiza haja ya kukabiliana na mzozo wa kifedha katika nchi zinazoendelea, na kufungua kwa haraka rasilimali zote zinazowezekana ili kuimarisha ulinzi wa kijamii na kusaidia wakulima wadogo na wa familia kuongeza tija na kujitegemea.