Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kuheshimu urithi ulioachwa na Nelson Mandela
2022-07-19 08:37:58| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemwelezea Hayati Nelson Mandela kama dira ya uadilifu, na kutoa wito wa kuheshimu urithi ulioachwa na rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Amesema Hayati Mandela anaendelea kuwa dira ya uadilifu na mfano wa kuigwa, na kuongeza kuwa Mandela alionyesha kuwa kila mtu ana uwezo na wajibu wa kujenga hatma nzuri kwa wote.

Ameongeza kuwa, njia bora ya kumuenzi Hayati Mandela ni kuheshimu urithi wake na kuutekeleza kwa vitendo.

Novemba 2009, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 18 Julai kuwa Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa kutambua mchango uliotolewa na rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini katika amani na uhuru.