Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa kimataifa wa turathi za kilimo
2022-07-19 08:38:39| CRI


Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Kimataifa wa Turathi Muhimu za Utamaduni wa Kilimo, uliofanyika katika wilaya ya Qingtian mkoani Zhejiang, China.

Kwenye barua yake Rais Xi amesisitiza kuwa, binadamu walianzisha ustaarabu mkubwa wa kilimo katika historia ndefu, na kulinda turathi za utamaduni wa kilimo ni jukumu la pamoja la binadamu. Amesema China imeitikia kwa hatua madhubuti pendekezo la Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, na kuhimiza ulinzi wa turathi muhimu za utamaduni wa kilimo siku hadi siku.

Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa kuimarisha ulinzi wa turathi za utamaduni wa kilimo, na kuendelea kutafuta thamani zake katika uchumi, jamii, utamaduni, ikolojia na teknolojia.