China yaimarisha sera yake ya kufungua mlango bila kuyumba
2022-07-20 08:50:33| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema uchumi wa China umeunganishwa kwa kina na dunia, na China itaendeleza sera yake ya kufungua mlango zaidi kwa nchi za nje.

Bw. Li amesema hayo jana kwenye mazungumzo maalum ya wajasiriamali duniani katika Baraza la Uchumi la Kimataifa yaliyofanyika kwa njia ya mtandao. Amesema maendeleo ya China hayatenganishwi na dunia, na maendeleo ya dunia pia yanaihitaji China. Ameongeza kuwa, China itaendelea kufungua mlango kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea, kulinda kwa pamoja mfumo wa biashara wa pande nyingi ambao kiini chake ni Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO), na kukuza biashara huria na biashara ya haki.