Idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan yafikia 105
2022-07-20 08:51:35| CRI

Idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya kikabila katika mkoa wa Blue Nile nchini Sudan imeongezeka na kufikia 105, na wengine 225 kujeruhiwa.

Katika taarifa yake, Mkuu wa Kurugenzi ya Masuala ya Dharura ya Afya na Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko katika Wizara ya Afya mkoani humo Omer Adam Omer amesema, miongoni mwa majeruhi, 20 wako katika hali mbaya, na wamehamishiwa katika hospitali ya mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, kwa ajili ya matibabu, huku watu wengine 8,470 wakikimbia makazi yao.

Hivi karibuni, mapigano makali yalizuka kati ya watu wa kabila la Hausa na Berta katika maeneo mengi ya mkoa wa Blue Nile kufuatia mauaji ya mkulima mmoja katika eneo la Gisan mkoani humo.