Rais wa Algeria atarajia kukuza mawasiliano na ushirikiano na China
2022-07-20 09:17:14| CRI

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesema nchi yake inatarajia kukuza mawasiliano na ushirikiano na China katika sekta mbalimbali.

Rais Tebboune ameyasema hayo alipokutana na balozi mpya wa China nchini Algeria Li Jian. Amesema Algeria inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano kati yake na China, na inatarajia kushirikiana na China kupanua mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kuhimiza uhusiano wao kuwa wa kiwango cha juu zaidi.

Balozi Li amesema China na Algeria zimeungana mkono na kutendana kwa dhati tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi, na ushirikiano wao katika sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Algeria kuendelea kuimarisha urafiki wao wa jadi, na kutia nguvu mpya kwa uhusiano wao wa wenzi wa kimkakati katika pande zote.