Marais wa Iran, Russia na Uturuki wafanya mazungumzo kuhusu suala la Syria
2022-07-20 08:54:03| CRI

Marais wa Iran, Russia na Uturuki walifanya mazungumzo jana usiku huko Tehran, mji mkuu wa Iran, ambapo walibadilishana maoni kuhusu suala la Syria chini ya mfumo wa Mchakato wa Astana. 

Habari kutoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran zimesema, taarifa ya pamoja iliyotolewa na pande hizo tatu imesisitiza kazi ya uongozi ya mchakato wa Astana katika ufumbuzi wa amani wa mgogoro unaoendea nchini Syria, kusisitiza ahadi thabiti kwa mamlaka ya nchi, uhuru na umoja, na ukamilifu wa ardhi pamoja na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa. Pia marais hao wameeleza nia yao ya kuendelea na mapambano ya pamoja dhidi ya ugaidi wa aina zote, na kusisitiza kuwa wanaamini kuwa mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kijeshi.