China yasema jumuiya ya kimataifa inafahamu chanzo cha msukosuko wa chakula
2022-07-20 09:11:37| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian ameitaka Marekani itafakari jukumu lake katika msukosuko wa chakula duniani, badala ya kuilaumu China.

Zhao Lijian amesema hayo kutokana na kauli iliyotolewa na mkurugenzi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa la Samantha Power, ambaye awali alisema kuwa, kuweka vizuizi kwenye biashara ya mbolea na kuhodhi chakula kwa China ni moja ya sababu za uhaba wa chakula katika Pembe ya Afrika.

Bw. Zhao amesema, China ni nchi iliyotoa fedha nyingi zaidi, kutuma wataalamu wengi zaidi na kukuza miradi mingi zaidi chini ya mfumo wa ushirikiano kati ya Kusini na Kusini, na jamii ya kimataifa inafahamu chanzo cha msukosuko wa chakula duniani.