China yasema Marekani ni nchi yenye idadi kubwa zaidi inayoshughulika na biashara ya uuzaji na usafirishaji wa watu duniani
2022-07-21 08:36:57| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema, kila mwaka Marekani inatengeneza ripoti isiyo na ukweli kuhusu suala la biashara ya uuzaji na usafirishaji wa watu, huku ukweli ukionyesha kuwa, Marekani ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi inayoshughulika na uuzaji na usafirishaji wa watu duaniani.

Bw. Wang amesema, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilikadiria kuwa, kila mwaka idadi ya watu waliosafirishwa nchini humo na kulazimishwa kufanya kazi ilifikia laki moja. Katika miaka 5 iliyopita, majimbo 50 na eneo maalumu la Colombia yote yaliripoti kesi za kulazimishwa kazi na uuzaji na usafirisha wa watu.