Watu 8 wauawa katika mashambulizi ya makombora kaskazini mwa Iraq
2022-07-21 08:35:43| cri

Watu 8 wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika shambulizi la makombora dhidi ya bustani ya mapumziko katika mkoa wa Dohuk wa eneo linalojiendesha la Wakurdi, kaskazini mwa Iraq.

Rais wa Iraq Barham Salih, kupitia mtandao wake wa kijamii, amelaani mashambulizi mapya ya makombora yanayofanywa na Uturuki kaskazini mwa Iraq.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imetoa taarifa ikikanusha madai hayo na kusema shambulio hilo ni la kigaidi. Wizara hiyo imesema, Uturuki iko tayari kuchukua hatua zote ili kujua ukweli na kupenda kushirikiana na Iraq kuwasaka wahusika.