Rais Xi Jinping wa China atoa barua ya pongezi kwa Kongamano la Baraza la Maendeleo la Vijana la Dunia
2022-07-21 15:56:57| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa barua ya pongezi kwa Kongamano la Baraza la Maendeleo la Vijana la Dunia

Rais Xi amesema vijana wanawakilisha matumaini, na vijana wataijenga kesho. Amesema China siku zote inawachukulia vijana kama nguvu hai inayohimiza maendeleo ya kijamii, huku ikiwatia moyo kuonesha ujana na uhai katika kushiriki kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Amelitaka baraza la maendeleo la vijana la dunia kuwa jukwaa muhimu la vijana kusaidia maendeleo ya dunia, na dunia nzima kuhimiza maendeleo ya vijana ili kutoa sauti ya vijana kwa umoja wa dunia na kutia nguvu ya ujana katika maendeleo ya dunia.