Rais wa Marekani aambukizwa COVID-19
2022-07-22 08:34:11| cri

Ikulu ya Marekani jana ilitangaza kuwa, rais wa nchi hiyo Joe Biden amethibitishwa kuambukizwa COVID-19, na alikuwa na dalili ndogo.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bi. Karina Jean-Pierre amesema, rais Biden ameanza matibabu na atawekwa karantini katika Ikulu na kuendelea na kazi zake kikamilifu.

Habari zinasema, rais Biden amepata dozi kamili za chanjo ya COVID-19 na dozi mbili za nyongeza.