Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Kimataifa la Maendeleo ya Vijana
2022-07-22 11:05:37| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Kimataifa la Maendeleo ya Vijana uliofunguliwa Alhamisi hapa Beijing.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesema vijana ni matumaini, na wanajenga mustakabali, na China siku zote inawachukulia vijana kama nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya jamii, na kuwahamasisha kuonesha uwezo wao katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Ameeleza matumaini yake kuwa, Kongamano hilo litakuwa jukwaa muhimu la kuhimizana kwa ajili ya maendeleo ya vijana na maendeleo ya dunia.

Rais Xi amesisitiza kuwa, vijana wa nchi mbalimbali wanapaswa kueneza thamani ya pamoja ya binadamu wote ya amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru, na kuchukua hatua halisi ili kusukuma mbele mapendekezo ya kuhimiza mendeleo ya dunia, na utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.