Mali yamtaka msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka ndani ya saa 72
2022-07-22 08:34:59| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali imemtaka msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA) kuondoka nchini humo ndani ya saa 72 kufuatia ujumbe kupitia mtandao wa kijamii kuhusu tukio la kidiplomasia kuongeza mvutano kati ya pande hizo mbili.

Wiki iliyopita, Mali ilitangaza kusitisha kwa muda mizunguko yote ya Tume hiyo kwa sababu za kiusalama. Tangazo hilo lilikuja siku chache baada ya mamlaka nchini humo kuwakamata askari 49 kutoka Cote d’Ivoire kwa madai kuwa wameingia nchini humo bila ruhusa.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatano wiki hii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali imemtuhumu msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo, Olivier Salgado kwa jumbe zake kwenye mtandao wa Twitter akisema bila ya ushahidi kuwa mamlaka za Mali ziliarifiwa awali kuhusu kuwasili kwa askari hao 49.