Mvua kubwa zilizonyesha nchini Pakistan zasababisha vifo vya watu 282
2022-07-22 08:40:46| cri

Mamlaka ya usimamizi wa maafa nchini Pakistan (NDMA) jana imetangaza kuwa, watu 282 wamefariki na wengine 211 kujeruhiwa tangu tarehe 14 mwezi Juni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha nchini humo.

Ripoti iliyotolewa na NDMA imesema, wanawake na watoto 160 ni miongoni mwa watu hao waliofariki, na kuongeza kuwa, mvua hizo zimeharibu nyumba zaidi ya 5,500, madaraja kadhaa na maduka nchini humo.