Roketi iliyobeba moduli ya maabara ya Wentian yarushwa mkoani Hainan
2022-07-24 15:20:05| cri

Roketi ya Long Macrch-5B Y3, iliyobeba moduli ya maabara ya Wentian ya kituo cha anga ya juu imerushwa leo Jumapili katika Eneo la Kurushia Roketi lililoko katika mkoa wa Hainan, China.

Moduli hiyo itabeba vifaa vipya, mikono ya roboti na nyenzo za kufanyia majaribio juu ya athari za anga ya juu kwa wanyama na mimea.