Rais wa Iran ataka manufaa ya kiuchumi ya nchi hiyo yahakikishwe kama makubaliano ya nyuklia yakifufuliwa
2022-07-25 09:20:01| CRI

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema, kama mazungumzo ya kurejesha utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA yataweza kufikia mwafaka au la, inategemea utatuzi kamili wa suala la uhakikisho wa kinyuklia, na vilevile kuhakikisha pande zote husika zinatekeleza makubaliano ipasavyo na Iran inapata manufaa ya kiuchumi.

Rais Raisi amesema hayo wakati akizungumzana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na kuongeza kuwa vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran vitaleta athari mbaya kwa uchumi wa dunia hususan kwa Ulaya. Rais Raisi amesema, uamuzi uliopitishwa na Bodi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) mwezi uliopita wa kuishutumu Iran kwa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa shirika hilo “sio wa kiujenzi”.