Moduli ya maabara ya Wentian yaungana na moduli kuu ya Tianhe ya kituo cha anga za juu cha China
2022-07-25 08:39:38| CRI

Shirika la Kupeleka Wanaanga kwenye Anga za Juu la China CMSA, limesema, moduli ya kwanza ya maabara ya kituo cha anga za juu cha China, imeungana kwa mafanikio na moduli kuu ya Tianhe.

Moduli ya Wentian, iliyorushwa Jumapili alasiri, imetia nanga kwenye moduli kuu ya Tianhe saa 9 na dakika 13 leo alfajiri kwa saa za Beijing, baada ya kuingia kwenye mzunguko uliopangwa na kukamilisha kurekebisha hali yake katika mchakato uliochukua karibu saa 13.

CMSA imesema, hii ni mara ya kwanza kwa vyombo viwili vya anga za juu vya China vyenye uzito wa zaidi ya tani 20 kukutana na kuungana kwenye mzunguko, na pia ni mara ya kwanza kwa vyombo hivyo kukutana na kuungana wakati wanaanga wakiwa kwenye kituo cha anga za juu.

Baadaye, wanaanga wa Shenzhou-14 wataingia kwenye moduli ya Wentian kama ilivyopangwa.