Mkutano wa kwanza wa baraza la utamaduni la Beijing wafunguliwa Beijing
2022-07-26 09:12:55| CRI


Mkutano wa kwanza wa baraza la utamaduni la Beijing umefunguliwa mjini Beijing na kuhudhuriwa na wakuu kutoka idara za serikali na utamaduni, wataalamu, wasomi, waandishi maarufu, wasanii na wafanyakazi wa utamaduni, ambao wamejadili mada mbalimbali.

Baraza hilo ambalo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Kuhimiza uvumbuzi wa kitamaduni, Kuwezesha maisha bora”, limeandaliwa na ofisi ya kikundi cha kuhimiza uongozi na ujenzi wa kituo cha utamaduni cha China na idara ya utangazaji ya kamati ya mji wa Beijing.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, naibu mkuu wa idara ya utangazaji ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China (CPC) ambaye pia ni waziri wa utamaduni na utalii Bw. Hu Heping amesema, China inatakiwa kufanya juhudi kuendeleza utalii wa umma, utalii wa kisasa, utalii wa kijani, na utalii wa ustaarabu, ili kukidhi mahitaji tofuati ya watalii.