Bw. Li Junhua kutoka China ateuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa UM anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii
2022-07-26 09:13:27| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres Jumatatu wiki hii amemteua Bw. Li Junhua kutoka China kuwa naibu katibu mkuu mpya anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii.

Bw. Li, ambaye kwa sasa ni balozi wa China nchini Italia na San Marino, atachukua nafasi ya Liu Zhenmin wa China.