China yatoa wito wa kuitishwa mkutano wa kimataifa kuhimiza mchakato wa amani katika Mashariki ya Kati
2022-07-27 09:26:50| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang amesema, China inatoa wito wa kuitishwa mkutano mkubwa zaidi wa kimataifa wenye ushawishi zaidi utakaoshirikisha nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wadau wote na mchakato wa amani katika Mashariki ya Kati.

Bw. Geng amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina. Amesema uamuzi husika wa Umoja huo juu ya suala hilo bado haujatelekezwa, haki halali za watu wa Palestina bado zinaendelea kudhulumiwa, na mchakato wa amani wa eneo hilo umesitishwa. Amesema Palestina na Israeli zinapaswa kutafuta njia za kuishi pamoja kwa amani, na jamii ya kimataifa inapaswa kutilia maanani kwa usawa ufuatiliaji wa pande hizo mbili juu ya masuala ya usalama.

Bw. Geng aliongeza kuwa China inaunga mkono nchi za Mashariki ya Kati na watu wao kushirikiana kwenye juhudi za kutatua masuala ya usalama wa eneo hilo na kutafuta njia za maendeleo kwa kujitegemea.