Ethiopia na AfDB zasaini makubaliano mawili ya mkopo
2022-07-28 08:48:59| CRI

Wizara ya Fedha nchini Ethiopia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimesaini makubaliano mawili ya mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 44.4.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo, mkopo huo ni kwa ajili ya miradi miwili inayolenga usalama wa chakula na ujenzi wa uwezo.

Taarifa hiyo imesema, mradi wa kwanza ni wa dola za kimarekani milioni 40 utakaofadhili utekelezaji wa mpango wa kujenga usalama wa chakula na lishe, na mradi wa pili wa dola za kimarekani milioni 4.4 zitatumika kutekeleza mpango wa kuimarisha usimamizi wa uchumi mkuu.

Mikopo hiyo inalenga kuboresha Amani na usalama katika maeneo ya chini nchini Ethiopia yanayokabiliwa na ukame kupitia kilimo imara na pia kuimarisha uwezo wa taasisi muhimu za kiuchumi.