Rais wa China asisitiza kushikilia ujamaa wenye umaalumu wa kichina ili kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa
2022-07-28 08:36:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kushikilia ujamaa wenye umaalumu wa kichina na kujitahidi kuandika ukurasa mpya katika kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi, ametoa kauli hiyo kwenye semina ya maofisa wa ngazi ya mikoa na wizara iliyofanyika kuanzia Jumanne hadi Jumatano mjini Beijing.

Akisisitiza umuhimu wa Mkutano wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika katika wakati muhimu kwenye safari mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, Rais Xi amesema malengo, majukumu na sera kwa ajili ya shughuli za Chama na Taifa katika miaka mitano ijayo na zaidi vitaamuliwa kwenye mkutano huo.