Marais wa China na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
2022-07-29 08:47:04| CRI

Rais Xi Jinping wa China Alhamisi usiku alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Joe Biden, ambapo walibadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala wanayoyafuatilia kwa pamoja.

Rais Xi alibainisha kuwa katika dunia ya leo, mielekeo ya mtikisiko na mabadiliko inaendelea kubadilika, huku upungufu wa maendeleo na usalama ukiendelea kuongezeka. Ili kukabiliana na dunia ya sasa inayojaa mabadiliko na machafuko, jamii ya kimataifa na watu wa sehemu mbalimbali duniani wanazitarajia China na Marekani, zikiwa nchi kubwa kiuchumi duniani, kuchukua nafasi ya uongozi katika kudumisha amani na usalama duniani na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia nzima. 

Rais Xi amesema, pande hizo mbili zinahitaji kudumisha mawasiliano kwenye ngazi zote na kutumia vyema njia zilizopo za mawasiliano ili kuhimiza ushirikiano kati yao.