Rais wa China asema U-marx unaonesha uhai mpya katika karne ya 21
2022-07-29 08:47:39| CRI

Rais Xi Jinping wa China Alhamisi alisema kuwa U-marx umeonesha uhai mpya katika karne ya 21, na kutoa wito kwa vyama vyote vya kisiasa vinavyofuata nadharia ya U-marx kuifanya nadharia hiyo ihusiane zaidi na hali ya kitaifa na zama za leo. 

Rais Xi aliyasema hayo kwenye ujumbe wa pongezi alioutoa kwa mkutano wa Baraza la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Vyama vya Kisiasa vinavyofuata U-marx Duniani uliofanyika hapa Beijing. 

Rais Xi amesema, U-marx ni nadharia iliyo wazi na inayoendelea, na pale tu inaporekebishwa kulingana na hali mahususi ya kila nchi ndipo inaweza kukita mizizi, na pale tu inapoendana na wakati ndipo inaweza kujaa uhai. 

Rais Xi amebainisha kuwa, U-marx katika karne ya 21 umekuwa ukifungua upeo mpya na kuzidi kuonesha uhai wake mpya, kutokana na juhudi za pamoja za vyama vya kisiasa vinavyofuata U-Marx katika nchi zote.