Xi asisitiza kuhimiza mshikamano wa watu wa nchini na wanaoishi nje kwa ajili ya ustawishaji mkubwa wa Taifa la China
2022-08-01 09:32:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuhimiza mshikamano wa watu wa nchini na wanaoishi nje na kufanya juhudi za pamoja ili kuongeza nguvu ya kustawisha taifa la China.

Katika mkutano wa kazi ya kamati kuu ya Chama ya kuunganisha watu uliofanyika Ijumaa hadi Jumamosi hapa Beijing, rais Xi akitoa hutuba amesema, mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 100 tangu chama cha CPC iweke kwa uwazi sera za kuunganisha watu , na amesititiza umuhimu wa kufuata njia sahihi ya maendeleo ya kazi ya kuunganisha watu wa uzalendo.

Akitaja kazi za msingi ya kuunganisha watu wa uzalendo katika zama mpya, rais Xi ametoa wito wa kushikilia uongozi wa CPC, kufuata njia ya ujamaa wenye umaalumu wa China, kuunganisha watu kwa kauli moja na kwa aina mbalimbali, na kuhimiza uhusiano wa masikilizano kati ya vyama vya kisiasa, makabila madogomadogo, dini, uhusiano wa watu wa ngazi tofauti wa kijamii pamoja na watu wa nchini na wanaoishi nje ya nchi.