Watu 32 wauawa katika shambulizi la uchomaji moto Madagascar
2022-08-01 09:29:18| CRI

Waziri wa Ulinzi wa Taifa wa Madagascar Richard Rakotonirina amethibitisha kuwa jumla ya watu 32 wameuawa katika shambulizi la uchomaji moto lililotokea Ijumaa katika kijiji cha wilaya ya Malagasy ya Ankazobe, ambacho kiko kilomita 100 magharibi ya mji mkuu Antananarivo.

Ndege na helikopta zimehamasishwa kusaidia kuwasaka wahusika wa ukatili huu ambao umesababisha vifo vya watu thelathini na wawili, na wengine wanne kujeruhiwa.

Washambuliaji hao walijihami kwa bunduki tatu aina ya AK-47, bunduki moja aina ya MAS-36 na shotgun nane na kuchoma nyumba hiyo kutoka ghorofa ya chini. Waliwafungia wahanga na kuwapiga risasi wale waliojaribu kukimbia.

Rais Andry Rajoelina wa Madagascar ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga na kulaani kitendo hicho, akitangaza kuwa waliofanya uhalifu huo wanasakwa na wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.