Wizara ya Ulinzi yasherehekea maadhimisho ya miaka 95 ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China
2022-08-01 09:30:41| CRI

Rais Xi Jinping jana Jumapili alishiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ambayo inaangukia leo Agosti Mosi.

Mbali na Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya kijeshi (CMC), viongozi waandamizi wa chama na serikali akiwemo waziri mkuu Li Keqiang pia walishiriki kwenye sherehe hizo zilizoandaliwa na wizara ya ulinzi ya China.

Akitoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama, mjumbe wa Kamati Kuu ya Kijeshi, ambaye pia ni mjumbe wa taifa na waziri wa ulinzi Wei Fenghe alitoa salamu kwa maafisa na askari wote wa jeshi la ukombozi wa umma la China, jeshi la polisi na wengineo. Wei pia alitoa heshima kwa wapiganaji wazee, wastaafu, na mashujaa waliochangia kwenye ujenzi na maendeleo ya jeshi la ukombozi wa umma la China na wajumbe wa wanajeshi wa mfano wa kuigwa . Pia alitoa salamu kwa watu wanaojitolea muda wao na kuwa mstari mbele kwenye viwanda vya sayansi na teknolojia za ulinzi wa nchi.

Wei ameeleza kuwa katika miaka 95 iliyopita, chini ya uongozi imara wa CPC, jeshi la PLA limepata mafanikio makubwa katika kuleta uhuru wa nchi , ukombozi wa watu na kuifanya nchi istawi na kuwa na nguvu.