Wizara ya Mambo ya Nje ya China yalaani ziara ya Pelosi mkoani Taiwan
2022-08-02 23:20:58| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku ya Jumanne ililaani vikali ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi katika mkoa wa Taiwan nchini China kwa kupuuza maonyo makali kutoka China.

Wizara hiyo imesema ziara ya Pelosi imetuma "ishara zisizo sahihi" kwa makundi ya ufarakanishaji yanayotaka" Taiwan ijitenge", na kuongeza kuwa imewasilisha malalamiko na pingamizi kali kwa upande wa Marekani.